KHAMIS DACOTA AFIWA NA MAMA YAKE MZAZI, MAZISHI JUMAPILI MCHANA


Mdau mkubwa wa muziki na mtangazaji wa vipindi vya muziki wa kiafrika kupitia Clouds FM na Clouds TV, Khamis Dacota amefiwa na mama yake mzazi Bi  Hindu Khamis Wazir Mwenda. (pichani juu).

Mama huyo ambaye hivi karibuni alichaguliwa kuwa mbunge wa viti maalum kupitia CUF, alifariki ghafla jana (Ijumaa 1/9/2017) jijini Dar es Salaam na atazikwa kesho Jumapili.

Khamis Dacota ameiambia Saluti5 kuwa msiba uko Kigamboni Kibada jirani kabisa na Shule ya Msingi Kibada ambapo mazishi yatafanyika katika makaburi ya Kisutu kesho mchana.

Kabla ya kuelekea Kisutu, mwili utapelekwa msikiti wa Manyema Kariakoo kwaajili ya kuswaliwa swala ya mwisho saa 7 mchana na kisha ndipo itawadia safari ya kuelekea makaburini.

No comments