KICHUPA CHA "MOYO KAMA MACHO" YA KIVURANDE JUNIOR HICHOO

HII inaweza kuwa taarifa murua masikioni mwa mashabiki wa muziki wa mduara, hususan wale waliokipokea kwa mikono miwili kibao ‘Moyo Kama Macho’ cha mfalme wa Kibao Kata, Jumaa Kivurande ‘Kivurande Junior’.

Taarifa yenyewe ni kuwa, video ya wimbo huo ambao kwa sasa unaonekana kuwa habari ya mujini baada ya kukubalika zaidi kila kona ya Tanzania, imekamilika na wakati wowote inaweza kumwagika mtaani.

Akiongea na Saluti5, Jumaa Kivurande amesema kuwa, video hiyo ambayo picha zake zimechukuliwa maeneo ya Dar es Salaam, Tanga na Mombasa, Kenya na ambayo iko katika ubora wa hali ya juu, imepangwa kuachiwa mwishoni mwa mwezi huu.

“Nawaomba mashabiki wangu wote wakae mkao wa kuusubiri kwa hamu ujio wa video hiyo kali na ya kisasa zaidi unaokuja kwa kishindo kikubwa sana,” amesema Kivurande ambaye wengi hupenda kumwita ‘Sukari ya Warembo’ kutokana na kuwa kivutio kikubwa kwa watoto wa kike.

No comments