KICK BOXING KUPELEKA WACHEZAJI MAFUNZONI NJE YA NCHI

MSIMAMIZI wa mchezo wa Kick Boxing, Japhet Kaseba amesema wameandaa mikakati ya kupeleka wachezaji nje ya nchi kwa ajili ya mafunzo.

Kaseba amesema kwamba sanjali na hilo pia wako katika maandalizi kwa ajili ya kushiriki mashindano mbalimbali ya kimataifa ili kujenga uwezo na kukuza mchezo huo.

Msimamizi huyo alisema tayari mchezaji mmoja, Jeremiah Naasari yuko mafunzoni nchini Malaysia kama sehemu ya maandalizi ya kwanza ya wachezaji hao.

Alisema kuwa matarajio ni kupeleka vijana wengine huko ili waweze kuungana pamoja katika kuukuza na kuuendeleza mchezo huo.

Kaseba alisema kuwa walipata fursa hiyo nchini humo kwa nia ya kuisapoti Tanzania kusonga mbele katika mchezo huo.
“Tumepata nafasi ya kipekee nchini humo kw a ajili ya kupeleka vijana kimafunzo, hivyo tutatumia nafasi ya kupeleka wachezaji wetu kulingana na idadi tutakayopata,” alisema Kaseba.


Msimamizi huyo alisema kuwa mafunzo hayo yatasaidia vijana kupata uzoefu wa kushiriki mashindano ya kimataifa.

No comments