KIUNGO WA NAPOLI AJUTIA KUSHINDWA KUKAMILISHA KUTUA MAN UNITED

KIUNGO wa timu ya Napoli, Marek Hamsik mwenye miaka 30, amejuta kushindwa kufanikisha uhamisho wa kutua katika kikosi cha Manchester United baada ya dirisha kufungwa.

Kiungo huyo ameripotiwa akisema kuwa ilikuwa nafasi muhimu kwake kutimiza ndoto ya kuchezea kwenye klabu kubwa lakini mambo yaliharibika dakika za mwishoni.


Manchester United iliachana na mpango huo baada ya kukamilisha usajili wa Nemanja Matic aliyegeuka kipenzi cha mashabiki wa timu hiyo.No comments