KLOPP AKIRI KUWA UKUTA WA LIVERPOOL UNAVUJA


Kocha wa Liverpool Jurgen Klopp amekiri kuwa Liverpool inaruhusu magoli mengi na hilo limekuwa jambo gumu kwake.
Hata hivyo kocha huyo amesema anakiamini na kukupenda kikosi chake na anafanya juu chini kuhakikisha kinakaa imara katika kila idara.
Klopp anasema: "Naipenda hii timu. Pengine kuna watu fulani wasiopenda, lakini mimi napenda na nafanya juhudi kuimarisha kikosi changu.
"Wakati mwingine unahitaji ngumi ya uso ili uzinduke na tayari tumeshapata kadhaa. Sio nzito sana, lakini ya Manchester City ilikuwa nzito. Ile ilikuwa ngumi pekee nzito.
"Hatukuanguka sakafuni, tuko hapa na tunacheza soka zuri, napenda namna timu inavyocheza ingawa ni kweli tunaruhusu magoli mengi. Ni jambo gumu lakini tunalifanyia kazi".

No comments