KOCHA POCHETTINO ATETEA ISHARA YA KIDOLE CHA KATI CHA DELE ALLI …asema hata Mr Bean hufanya hivyo


Kocha wa Tottenham Mauricio Pochettino anaamini FIFA itakosea iwapo itamwadhibu Dele Alli kwa ishara yake ya kidole cha kati alichoonyesha kwenye mchezo dhidi ya England Slovakia.

Kocha huyo akatania kwa kumlinganisha nyota huyo na mchekeshaji wa Uingereza Mr Bean.

Alli alishutumiwa kuwa alidhamiria kumtusi refa Clement Turpin lakini mwenyewe akadai kuwa alikuwa akitaniana na mchezaji mwenzake na swahiba wake mkubwa Kyle Walker.

Picha zilizoonyeshwa kwenye runinga zilimuonyesha Alli akionyesha ishara hiyo dakika ya 77 siku ya Jumatatu walipopata ushindi wa 2-1 katika uwanja wa Wembley.

''Kuyaweka bayana, ishara hiyo ilikuwa ni ya utani kati yangu na rafiki yangu Kyle Walker,'' Alli, 21, alichapisha kwenye mtandao wake wa Twitter.''Naomba msamaha kwa kosa lolote lililotendeka.''

Shirikisho la kandanda duniani (Fifa) linasubiri ripoti kutoka kwa viongozi wa mechi hiyo, inayotarajiwa kutolewa mwishoni mwa wiki, kabla ya kutoa maamuzi iwapo kumfungulia mchezaji mashtaka kwa ukosefu wa nidhamu au la.

Alli na beki Walker walikuwa wakiichezea klabu ya Spurs hadi pale Walker alipojiunga na Manchester City majira ya joto.

Pochettino amesema: “Ilikuwa ni mzaha. Ni kweli sio ishara nzuri lakini si jambo linalostahili kukuzwa sana. Mtazame Mr Bean watu wote huchekeshwa nae kwa ishara kama hiyo.

“Dale alikuwa akitaniana na Kyle Walker! Hebu tuyaache hayo. Tupaswa kutatua hili kwa kumwangalia Mr Bean”.No comments