KUELEKEA DIMBA MUSIC CONCERT, KING KIKI, KAKERE WAMLIZA HUSSEIN JUMBE


MWANAMUZIKI nguli wa muziki dansi nchini, Hussein Jumbe (pichani) juzi alijikuta akimwaga machozi ya furaha wakati wa mazoezi ya pamoja na mastaa wenzake wanaounda kombaini ya dansi yaliyofanyika katika ukumbi wa CCM Mwinjuma Mwananyamala, jijini Dar es Salaam.

Tukio hilo lilitokea mara baada ya wanamuziki wenzake Kikumbi Mwanza Mpango na Juma Kakere kuingiza vipande vipya vya mashairi katika wimbo wa Jumbe 'Siri ya Nini' ambavyo vilimsisimua na kujikuta akilia kwa furaha.

"Kiki na Kakere wameniliza kwakweli sikutegemea kama wangeweza kunishtua kwa kiasi hiki kwa namna walivyoingiza hisia mpya kwenye wimbo huu na kuifanya iwe remix  tamu”, alisema Jumbe.

Mastaa hao dansi walikuwa kambini wakijifua kujiandaa na mpambano dhidi ya bendi ya Msondo Ngoma utakaofanyika Iddi Pili, Septemba 2 katika ukumbi wa Travertine, Magomeni jijini Dar es Salaam.

No comments