LIVERPOOL MAJI YA SHINGO KWA SEVILLA


Liverpool imelazimishwa sare ya 2-2 na Sevilla ya Hispania katika mchezo wa kundi E wa Champions League.

Kwa matokeo hayo Liverpool inakuwa timu pekee kutoka England iliyokosa ushindi katika mechi za kukata utepe hatua ya makundi wiki hii.

Wissam Ben Yedder aliitanguliza Sevilla kwa bao la dakika ya tano, Roberto Firmino akachomoa dakika ya 21 kabla Mohamed Salah hajaifungia Liverpool goli la pili dakika ya 37. Sevilla ilisawazisha kupitia kwa Joaquin Correa dakika ya 72.

LIVERPOOL (4-3-3): Karius 6.5; Gomez 7, Lovren 5.5, Matip 7, Moreno 8.5; Wijnaldum 7, Henderson 7, Can 7 (Coutinho 76); Salah 7 (Oxlade-Chamberlain 89), Firmino 8, Mane 8 (Sturridge 83)

SEVILLA (4-3-3): Rico 7; Mercado 6, Pareja 6, Kjaer 6, Escudero 7; N'Zonzi 6.5, Banega 7, Piazarro 6 (Sarabia 45, 6); Navas 5.5 (Corchia 83), Ben Yedder 6.5 (Muriel 69), Correa 7 No comments