Habari

LUKAKU AWEKA REKODI MPYA MANCHESTER UNITED …hakuna cha Cantona, Rooney, Ibrahimovic wala Ruud van Nistelrooy

on

Amekuwa mchezaji wa Manchester United kwa wiki chache, lakini Romelu Lukaku ameshatengeneza rekodi ambayo haikuwahi kufikiwa hapo kabla ndani ya kabla Old Trafford.
Mshambuliaji huyo wa Kibelgiji, alifunga mara mbili Jumatano usiku katika mchezo wa Champions League dhidi ya CSKA Moscow na kuendeleza makali yake.
Lukaku sasa amefunga magoli 10 katika mechi zake 9 za mwanzo za kimashindano ndani ya United kudhihirisha thamani yake ya pauni milioni 75.
Hapo kabla, hakuna mchezaji yeyote wa Manchester United aliyefunga idadi kama hiyo katika mechi 9 za mwanzo ndani ya msimu wa kwanza kwa United. Hii imefanywa kwa mara ya kwanza na Lukaku.
Kwa kufanya hivyo, Lukaku anavuka rekodi ya Bobby Charlton ya mwaka 1956 ya magoli tisa katika mechi tisa.

Comments

comments

About Saluti 5

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *