LWANDAMINA ADUWAZWA NA UWANJA WA NJOMBE, AISHANGAA TFF


KOCHA wa Yanga, George Lwandamina ameshangazwa na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), kuruhusu soka kuchezwa katika uwanja wa Sabasaba mkoani Njombe kisha akawaambia mashabiki wa Yanga “Tulieni, dozi za maana zinakuja.”

Akiongea na saluti5, Lwandamina alisema walikuwa katika wakati mgumu licha ya kushinda wakati wakipambana na Njombe Mji waliokuwa nyumbani kutokana na ubovu wa uwanja huo.

Lwandamina alisema Njombe haikuwa timu ya kuizuia na kwamba walipaswa kuwafunga kwa mabao mengi zaidi lakini kilichokwamisha ni uwanja huo mbovu.

Kocha huyo amesema, baada ya kugundua ubovu wa uwanja huo, aliamua kukibakisha kikosi chake kufanya mazoezi katika uwanja huo kwa ajili ya kuwaandaa wachezaji wake kwa mechi ambayo itapigwa wikiendi hii dhidi ya Majimaji.


“Sijui ni vipi wahusika wa soka nchi hii waliruhusu uwanja kama huu kuchezewa Ligi, hauna ubora kabisa. Tulipaswa kushinda mabao mengi lakini uwanja uliwasaidia wenzetu kutokufungwa nyingi,” alisema Lwandamina.


No comments