LWANDAMINA AKATISHA MSIBA WA BABA YAKE KUWAHI MAANDALIZI YA LIGI KUU

KOCHA wa Yanga, George Lwandamina amelazimika kusitisha maombolezo ya msiba wa baba yake ili kuwahi maandalizi ya Ligi, lakini alipotua jana usiku akawasili pamoja na beki mpya wa timu yake.

Lwandamina alirejea jana usiku akitokea kwaoNdola, nchini Zambia lakini akiwa jijini Nairobi akisubiri ndege ya kuunganisha kuja jijini Dar es Salaam alikutana na beki wake mpya, Kayembe Fiston.

Ingawa hawakujuana, kocha huyo alitua jijini Dar usiku na kukutana na mabosi wa timu hiyo wakija kumpokea beki wao huyo anayekuja kwa majaribio ya wiki mbili.

Kutoa kwa Fiston aliyeitumikia klabu ya SM Sanga Balende kutamfanya Lwandamina kuanza kumwangalia beki huyo katika majaribio hayo yanayoanza leo katika kikosi hicho.

Fiston anayekuja Yanga kwa majaribio kwa pendekezo la kiungo Papy Tshishimbi ambaye amewaambia mabosi wa Yanga kwamba beki huyo endapo watamalizana nae hakuna mshambuliaji wa timu pinzani atakayetamba mbele ya ukuta wa timu yao hiyo.

Wakati Lwandamina akitua jana usiku, mabosi wa klabu hiyo wanakutana nae leo katika hatua ya kumpa pole zaidi.

No comments