LWANDAMINA AWAACHIA AJIB, NGOMA JUKUMU LA USHINDI NJOMBE NA SONGEA

KOCHA wa timu ya Yanga, George Lwandamina raia wa Zambia ameliacha jukumu la kusaka pointi sita ugenini chini ya washambuliaji wake wazoefu, Ibrahim Ajib na Dornald Ngoma mzaliwa wa Zimbabwe.

Kocha huyo ambaye kikosi chake kimeachwa na Simba kwa alama mbili, alisema kuwa suala la kushinda mechi zote mbili mikoani halikwepeki na washambuliaji wake wanafahamu mtihani aliowapa kabla ya kuelekea mechi hizo kwenye miji ya Njombe na Songea.

Amesema kusudio lao ni kurudi Dar es Salaam na pointi sita anbazo zitawaongezea kasi ya kushinda mechi nyingine mbili watakazocheza nyumbani kabla ya kuwafata Kagera Sugar na Stand United Shinyanga.

"Hakuna namna nyingine tunayoweza kufanya zaidi ya kupambana katika kipindi hiki ambapo tuna baadhi ya wachezaji muhimu majeruhi,’’ alisema kocha huyo.


"Ntalazimika kuwatumia Ngoma na Ajib katika nafasi ya ushambuliaji, mwanzoni ilikuwa na ugumu kidogo lakini sasa wameanza kuelewana nadhani wanaweza wanaweza kufanikisha lengola kukusanya point ugenini,’’ aliongeza.

No comments