LWANDAMINA: MSIIHUKUMU YANGA KWA MATOKEO DHIDI YA LIPULI TU

KOCHA wa Yanga, George Lwandamina amesema kuwa anashangaa namna ambavyo watu wanaitoa Yanga katika mbio za kuwania ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara msimu huu.

Lwandamina amesema kuwa watu wamekuwa wakihukumu mwenendo wa timu kutokana na matokeo ya mchezo wa kwanza dhidi ya Lipuli, lakini hawafahamu namna walivyojipanga kuhakikisha wanarejea katika ubora wao.

“Najua namna ambavyo watu wanatufikiria kwa sasa, lakini hilo haliwezi kutusumbua kwa sababu sio kazi yetu kupima mitazamo ya watu, nadhani tunaweza kuwajibu kuanzia mechi inayofuata,” alisema kocha huyo.

“Kama kuna watu wanawaza kutuondoa katika mbio za kutetea ubingwa msimu huu basi wanajidanganya kwasababu sisi dhamira yetu iko palepale na hatuwezi kuyumbishwa na matokeo ya mchezo mmoja,” aliongeza.

“Mpira hautabiriki kwa sababu unaweza kuanza vizuri lakini mwisho wa msimu usiambulie kitu,” alimaliza.


Yanga iliyobeba ubingwa mara tatu mfululizo imeshacheza mchezo wake wa kwanza dhidi ya timu ya Lipuli ambayo imepanda daraja na kuambulia sare ya bao 1-1.

No comments