MABUSU YA RAMSEY NOAH YAMPAGAWISHA MREMBO WA NOLLYWOOD

STAA wa filamu za Nollywood, mrembo Omoni Oboli amesema kuwa kama kuna wanaume ambao wanamvutia kupiga busu wakati wa kuigiza ni Ramsey Noah.

Mrembo huyo pia amemtaja Dismond Eliot kama mwigizaji mwingine wa kiume  ambaye pia anamvutia kumpiga busu wakati wa maigizo.

‘’Ni kweli lile ni tendo la kuigiza lakini wakati mwingine kama wanadamu tunavutiwa na baadhi ya watu, binafsi Ramsey Noah anavutia kuigiza nae tendo la busu," amesema staa huyo.


Ramsey  anatajwa kuwa staa wa kiume mwenye mvuto wa kimapenzi nchini Nigeria na alijipatia umaarufu kupitia filamu ya "My Love."

No comments