MAINA BAND YAJINASIBU KUACHA SIMULIZI MASTERS CLUB JUMAMOSI HII

JUMAMOSI hii, kama kawaida ya Maina Band, burudani isiyo na mfano itaendelea kuunguruma ndani ya kiwanja chao cha kujidai cha Masters Club, jijini Dar es Salaam.

Bosi wa maina Band, Liston Maina ameiambia Saluti5  kuwa, tofauti na wiki nyingine zote, Jumamosi hii wataangusha muziki ambao wanaamini utaacha simulizi kwa mashabiki watakaofika kuburudika.


“Tunachoomba tu ni kwamba mashabiki wajitokeze kwa wingi ili kujifaidia burudani ya ukweli na iliyokwenda shule kwani kama kawaida yetu Maina Band ni raha tu,” amesema Liston. 

No comments