MAJERUHI GODFREY MWASHIUYA APANIA KUREJESHA MAKALI YAKE

KINDA wa timu ya Yanga, Godfrey Mwashiuya ambaye alikuwa moto wakati anasajiliwa amesema kuwa hivi sasa anaendelea vyema na yupo mbioni  kurejesha makali yake.

Mwashiuya amekuwa akisumbuliwa na jeraha la goti lililomuweka nje ya kikosi kwa muda mrefu.

Wakati anatua Yanga akitokea timu ya Kimondo FC alikuwa moto kiasi cha mashabiki kuanza kumfananisha na winga aliyekosa mfano hapa nchini, Edibily Lunyamila anayefanya kazi ya uchambuzi wa michezo hivi sasa.

"Nimeandaliwa program  maalumu ya mazoezi na benchi la ufundi na kadri siku zinavyozidi kwenda nimekuwa nikizidi kuimarika, naamini muda si mrefu nitarejea kwenye ubora wangu,’’ alisema Mwashiuya.

"Napata sapoti kubwa kutoka kwa kocha na benchi la ufundi kwa kipindi chote nilichokuwa nikisumbuliwa na jeraha lakini sasa naona kuna kila dalili ya kukaa sawa,’’ aliongeza.

"Ukiwa kama mchezaji shauku yako ni kuona unapata nafasi ya kucheza mara kwa mara lakini unapokaa nje ya kikosi kwa sababu ya jeraha huwa inaumiza kidogo,’’ alimaliza

No comments