Habari

MAKALI YA FABREGAS YAFUFUKA CHELSEA

on

Baada ya msimu uliopita kumalizika huku akiwa mchezaji kutokea benchi,  Cesc Fabregas amerejea kwenye makali yake na sasa ni moja ya majina ambayo hayakosekani kwenye kikosi kinachoanza cha  Antonio Conte.
Kiungo huyo wa Hispania mwenye umri wa miaka 30, amenufaika kwa kiasi kikubwa na kuondoka kwa Nemanja Matic aliyehamia Manchester United.
Msimu uliopita hakuweza kuanza hata mara moja katika michezo miwili mfululizo ya Premier League, lakini hadi sasa katika mechi zote saba za Chelsea za mashindano yote, amekosa mechi moja tu, tena kwa adhabu ya kulambwa kadi mbili za njano.
Katika mchezo wa Jumapili dhidi ya timu yake ya zamani, Arsenal ulioisha kwa sare ya 0-0, Fabregas alitengeneza nafasi nne za kufunga, idadi ambayo haikufikiwa na mchezaji mwingine yeyote yule kwenye mechi hiyo.

Comments

comments

About Saluti 5

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *