Sanabria alifunga bao la ushindi kunako dakika ya 94 huku Real Betis ikiishangaza Real Madrid na kupata ushindi katika uwanja wa Bernabeu kwa mara ya kwanza katika La Liga ndani ya  miaka 19.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 21 aliruka na kufunga bao tamu la kichwa  kufuatia krosi iliopigwa na Antonio Barragans.
Kikosi cha Zinedine Zidane kilitawala kipindi kirefu cha mechi, lakini Cristiano Ronaldo ni miongoni mwa wachezaji wa nyumbani waliopoteza fursa za kuiweka mbele Real Madrid huku klabu hiyo ikishambulia mara 27 bila kufaulu.
Hatua hiyo sasa inawawacha mabingwa hao wa Ulaya wakiwa pointi saba nyuma ya viongozi wa ligi Barcelona.
Hiyo ilikuwa mechi ya kwanza ya La Liga kwa Ronaldo  tangu amalize adhabu yake ya kufungiwa mechi tano. 
Rais wa Real Madrid Florentino Perez ambaye ameshuhudia timu yake ikishindwa kuvuna ushindi kwa mara ya tatu kwenye uwanja wake wa nyumbani, alilazimika kwenda katika vyumba vya kubadilishia nguo baada ya mechi kumalizika.
Hata hivyo inaaminika  Florentino Perez alichukua hatua hiyo kwa nia njema ya kuwapa moyo wachezaji na kocha Zinedine Zidane.

USISAHAU KUBONYEZA SUBSCRIBE HAPO
LIKE PAGE YETU YA FACEBOOK Saluti5

Post a Comment

 
Top
Nicolaus Trac