Habari

MAN UNITED MOTO CHINI …CSKA MOSCOW YAPEWA 4-1 …Lukaku hashikiki

on

CSKA Moscow imekubali kichapo cha bao 4-1 nyumbani dhini ya Manchester United ambayo iko katika kiwango cha kutisha msimu huu.
Katika mchezo huo wa Ligi ya Mabingwa, Romelu Lukaku aliifungia United mara mbili dakika ya 4 na 27 huku Anthony Martial akifunga dakika ya 19 kwa mkwaju wa penalti kabla Henrik Mkhitaryan aliyekuwa nyota wa mchezo hajahitimisha karamu ya magoli ya dakika ya 57.
Hata hivyo ‘gazeti’ la Manchester United likachafuka dakika ya 90 baada ya Konstantin Kuchaev kuifungia CSKA Moscow bao pekee.
CSKA Moscow (3-5-2): Akinfeev 6; Vasin 5, V Berezutsky 4.5, Ignashevich 5; Fernandes 6, Dzagoev 6.5 (Milanov 72), Wernbloom 5.5, Golovin 7, Schennikov 5.5; Chalov 5 (Zhamaletdinov 67), Vitinho (Kuchaev 90). 
Manchester United (3-4-3): De Gea 7; Bailly 6.5, Lindelof 6, Smalling 6; Young 6.5 (Darmian 67), Matic 6.5, Herrera 6, Blind 6; Mkhitaryan 8.5 (Lingard 60), Lukaku 8, Martial 8 (Rashford 72).

Comments

comments

About Saluti 5

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *