MANCHESTER UNITED YAANZA KWA USONGO CHAMPIONS LEAGUE KWA KUIKALISHA BASLE 3-0 ...Benfica yaanza vibaya kwa CSKA Moscow

Manchester United imeanza kwa usongo mkubwa Ligi ya Mabingwa baada ya kuichapa Basle ya Uswisi 3-0 katika mchezo mgumu wa kundi A.


Katika mchezo huo uliopigwa Old Trafford, United ikampoteza kiungo wake Paul Pogba kunako dakika ya 19 baada ya kuumia huku nafasi yake ikichukuliwa na Marouane Fellaini.

Na ni Fellaini huyo huyo ndiye aliyeifungulia njia Manchester United kwa kufunga bao la kwanza dakika ya 35 akiunganisha kwa kichwa krosi tamu ya Ashley Young.

Magoli mengine ya United yalifungwa kipindi cha pili kupitia kwa  Romelu Lukaku na Marcus Rashford.

MANCHESTER UNITED (4-2-3-1): De Gea; Young, Lindelof, Smalling, Blind; Matic, Pogba (Fellaini 19'); Mata (Rashford 77'), Mkhitaryan, Martial (Lingard 69'); Lukaku
Magoli: Fellaini 35', Lukaku 53', Rashford 85'

BASLE (3-4-3): Vaclik; Akanji, Suchy, Balanta; Lang, Xhaka, Zuff, Riveros Galeano (Oberlin 77'); Steffen, Van Wolfswinkel (Bua 66'), Elyounoussi.

Mchezo mwingine wa kundi A uliikutanisha Benfica ya Ureno iliyokalishwa 2-1 na CSKA Moscow ya Urusi.


No comments