Habari

MANCHESTER UNITED YAREJEA ANGA ZA 4-0 … Valencia, Mkhitaryan, Lukaku, Martial wainyamazisha Everton

on

Manchester United imeikung’uta Everton 4-0 kwenye mchezo mkali wa Ligi
Kuu ya England uliochezwa kwenye uwanja wa Old Trafford.
Antonio Valencia alifunga bao linalostahili kuingia kwenye mabao bora
ya msimu kwa shuti kali la dakika ya nne.
Matic alitoa pasi ndefu ya juu kutoka upande wa kushoto iliyoenda kwa
Valencia upande wa kulia ambapo beki huyo akiwa nje ya 18 akaungaunisha kwa
mkwaju mkali uliomshinda kipa Jordan Pickford.
Kipindi cha pili ndicho kilichokuwa na heka heka zaidi kwa pande zote,
lakini ni Manchester United iliyofanikiwa kupata magoli mengine matatu katika
dakika kumi za mwisho wa mchezo.

Henrik Mkhitaryan aliyepewa pande tamu na Lukaku alifunga bao la pili
dakika ya 83 huku Lukaku naye akitupia wavuni goli la tatu dakika ya 89 kabla Anthony
Martial hajafunga la nne dakika ya 90 kwa njia ya penalti.
Nahodha wa zamani wa Manchester United Wayne Rooney aliyejiunga na Everton, alishindwa kufurukuta na alipumzishwa dakika ya 82.
Hii ni mara ya tatu msimu huu kwa Manchester United kushinda 4-0 kwenye Premier League.
MAN UTD (4-3-3): de Gea, Valencia, Bailly, Jones, Young, Fellaini, Matic, Mata (Herreraat 77), Mkhitaryan (Martial 88), Rashford (Lingard 60), Lukaku 
EVERTON (3-4-3): Pickford, Keane, Jagielka, Williams, Martina, Schneiderlin, Gueye (Calvert-Lewin 76), Baines, Davies (Sandro 66), Sigurdsson, Rooney (Mirallas 81)

Comments

comments

About Saluti 5

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *