Habari

MANCHESTER UNITED YAWEKA REKODI MPYA YA MAPATO

on

Manchester United imetangaza faida ya pauni milioni 81 na mapato ya pauni
milioni 581 kwa kipindi cha fedha cha 2017 ambayo ni rekodi mpya. 
Katika mwaka mmoja baada ya kushinda kombe la Europa League na EFL
klabu hiyo imetia saini kandarasi 12 za ufadhili huku mapato ya matangazo
pamoja na yale yanaopatikana wakati wa mechi yakiongezeka.
Klabu hiyo ilifaidika kutoka kwa ongezeko la mapato ya televisheni
wakati wa kipindi cha 2016-17 ikiwa ndio mwaka wa kwanza kati ya mitatu ya
makubaliano ya matangazo ya televisheni.
Mnamo mwezi Juni tarehe 30 mapato ya matangazo yaliongezeka hadi pauni
milioni 194 kutoka pauni milioni 140 mwaka mmoja kabla ikiwa ni ongezeko la asilimia
38.
Msimu huu Manchester United  imerudi katika Ligi ya Mabingwa barani Ulaya,
hatua inayotarajiwa kuzidi kuinufaisha klabu hiyo kimapato.

Comments

comments

About Saluti 5

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *