MANGO GARDEN YASALIMIKA KWA MUDA …Mahakama yasitisha bomoa bomoa


Suala la ukumbi wa Mango Garden kuvunjwa limechukua sura mpya baada ya mahakama kutoa agizo la kuzuia hatua hiyo hadi hapo kesi ya msingi itakapokamilika.

Habari za ndani ambazo zimeifikia Saluti5 ni kwamba uongozi wa Mango Garden umepeleka shauri hilo mahakami ukihitaji kulipwa fidia na Umoja wa Vijana wa CCM kabla ukumbi haujavunjwa.

“Angalau kwa mwezi huu na mwezi ujao wote (Oktoba) tutendelea kuwepo hapa, kama kuna badiliko lolote basi labda ni baada ya hukumu ambayo haitegemiwi kutoka kabla ya mwezi Novemba mwaka huu,” anaeleza mtu wa ndani wa Mango Garden na kuongeza kuwa huduma zote zinaendelea kama kawaida.

No comments