MBARAKA YUSUPH AISUBIRI MECHI YAO DHIDI YA SIMBA KUTAFUTIA UJIKO ZAIDI

MSHAMBULIAJI mpya wa timu ya Azam, Mbaraka Yusuph anesema ataitumia mechi yao dhidi ya Simba kutangaza ukubwa wajina lake hapa nchini.

Mbaraka ametamba kuonyesha makali yake kwenye mchezo wa Jumamosi watakapoikabili Simba kwenye uwanja wa Azam Comprex, jijini Dar es Salaam kwa mara ya kwanza.

Mshambuliaji huyo amesema kuwa anataka kuendeleza rekodi yake ya kuifunga Simba kama walivyofanya msimu uliyopita na hakuna kikwazo ambacho kinaweza kumzuia asifanye hivyo.

"Nafurahi kwasababu mechi hiyo itachezwa kwenye uwanja wetu wa nyumbani, nakubali kuwa Simba ni timu kubwa lakini tutapambana nao na nitawafunga kama walivyozoea katika msimu uliyopita," alisema Yusuph.

Mshambuliaji huyo amesema baada ya kuwa majeruhi, sasa yupo fiti na amefanya mazoezi ya kutosha kuhakikisha anasaidia timu yake kuweza kufanya vizuri kwenye msimu huu ikiwezekana kuweza kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara.


"Kitu cha muhimu kwetu ni ushindi na ubingwa na hilo linawezekana kutokana na maandalizi ambayo tumeyafanya na mshikamano uliopo kwa wachezaji pamoja na viongozi, naamini kwa umoja huu hakuna ambacho kitashindikana kwani kila mmoja wetu anafanya kazi yake vizuri,’’ amesema.

No comments