MBOTO AWASHUSHUA WANAODAI BONGOMUVI IMEPOTEZA MWELEKEO

MKALI wa muvi za Kibongo ambaye ni hodari kwa kuvunja mbavu, Haji Salum “Mboto” ameendelea kupingana na wale wanaodai kuwa tasnia ya filamu imepoteza mwelekeo kwa kusema kuwa fani hiyo bado iko katika ubora wake.

Akiongea na Saluti5, Mboto amesema kuwa wanachoshindwa kutofautisha watu wengi ni uwezo mdogo wa uandaaji wa baadhi ya wasanii na ulipuaji katika kazi hiyo anayodai kwamba kwa sasa imevamiwa na watu wengi wasio na uwezo nao.

“Filamu Bongo bado iko katika chati na maneno kwamba imepoteza mwelekeo ni ya kujifurahisha tu ambayo baadhi ya watu wamekuwa wakizungumza, hasa wanapokosa la kufanya,” amesema Mboto.


“Lakini ukweli ndo huo ila kinachotakiwa kwetu wasanii wa muvi ni kuzidisha umoja na mshikamano na kuhakikisha tunaepuka kuandaa kazi za “zima moto” ili kujitengenezea heshima ambayo imeanza kupwaya,” ameongeza. 

No comments