Habari

MICHY BATSHUAYI AIPA CHELSEA USHINDI MUHIMU DHIDI YA ATLETICO MADRID

on

Michy Batshuayi amefunga bao muhimu na la ushindi kwa  Chelsea ambayo ilitoka nyuma na kuichapa Atletico Madrid 2-1 katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya uliochezwa kwenye uwanja wa Wanda Metropolitano.
Licha ya kucheza vizuri dhidi ya miamba hiyo ya Hispania, kikosi cha Antonio Conte kikaonekana kama vile kitaambulia sare.
Muda mfupi kabla  ya mapumziko, Antoine Griezmann alifunga bao la kuongoza kwa wenyeji kwa mkwaju wa penalti kufuatia faulo iliyofanywa na David Luiz, lakini Alvaro Morata akasawazisha dakika ya 60.
Wakati kila mtu akiamini kuwa mchezo unamalizika kwa sare, Michy Batshuayi akaifungia Chelsea bao la ushindi dakika ya mwisho ya mchezo.

Atletico Madrid (4-4-2): Oblak; Juanfran, Godin, Lucas, Filipe Luis; Koke, Thomas (Gimenez 77), Saul, Carrasco (Torres, 69); Correa (Gaitan 70), Griezmann
Chelsea (3-5-1-1): Courtois; Azpilicueta, David Luiz, Cahill; Moses, Bakayoko, Kane, Fabregas, Alonso; Hazard (Willian, 82); Morata (Batshuayi 82)

Comments

comments

About Saluti 5

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *