MITANDAO YA KIJAMII SASA YAMCHEFUA TONTO DIKEH


STAA wa filamu asiyeishiwa vituko nchini Nigeria, Tonto Dikeh ameonyesha kukerwa na mwenendo wa mitandao ya kijamii.

Tonto amesema kuwa hivi sasa hakuna tena usiri wa mambo binafsi kwasababu mitandao inaweka hadharani maisha binafsi ya watu.

“Kama kuna kitu kimeanza kunikera ni uwepo wa mitandao ya kijamii kwa sababu ya taarifa nyingi za kizushi zinazolenga kuchafuana,” alisema staa huyo.


“Ni kweli imesaidia kuunganisha watu lakini ile raha ya kuwa na usiri wa mambo yako ya ndani hivi sasa haipo tena, kila kitu kipo wazi,” aliongeza.

No comments