MKONGWE WA NOLLYWOOD AMPONDA GENEVIEVE

STAA mkongwe, Ego Boyo amekuwa kimya kwa muda mrefu baada ya kujiweka kando na kazi za sanaa lakini hivi karibuni ameibuka na kuanza kuponda baadhi ya mastaa wakubwa wa filamu nchini Nigeria.

Ego amesema kuwa baadhi ya mastaa akiwemo Genevive wameshindwa kufanya uhalisia katika filamu wanazocheza kiasi cha kukosa mvuto kama zile za zamani.

"Mandhali ya majumba mazuri na magari ya kifahari havisababishi filamu kuwa nzuri, kuwaza hivyo ni kujidanganya watu wanahitaji waigizaji halisi," alisema mkonwe huyo.


"Wapo wazoefu kama Genevive lakini sijui kwa nini wanakuwa feki mbele ya kamera kiasi cha kuanza kuboa,’’ aliongeza.

No comments