MMILIKI WA KISUMA BAR AFARIKI DUNIA …ngome ya Talent Band, Msondo na Sikinde


Mmiliki wa Kisuma Traders inayomili bar kibao za Kisuma zinazoongoza kwa ‘kuukarimu’ muziki wa dansi Fulgence Urio (pichani) amefariki ghafla Jumatatu usiku.

Kifo cha Urio ni pigo kubwa kwa muziki wa dansi hasa kutokana na ukweli kuwa amekuwa mfadhili wa bendi na wasanii wengi wa dansi akiwemo gwiji Hussein Jumbe.

Akiongea na Saluti5, Hussein Jumbe ambaye bendi yake ya Talent hupiga kila wiki kwenye bar za Kisuma Bar alisema Jumatatu asubuhi alikutana na Urio na kufanya naye maongezi marefu ofisini kwake akiwa mzima wa afya.

“Tuliongea mambo mengi, ikiwemo nia yake ya kutaka kumzawadia Said Mabela kwa kudumu kwake Msondo Ngoma kwa muda mrefu, lakini nilishtushwa usiku nilivyoambiwa Urio amefariki, anaeleza Hussein Jumbe.

Talent Band hupatikana Kisuma Bar Temeke Mwembeyanga kila Ijumaa na Jumapili huku Sikinde wakiwa hapo kila Jumamosi, bila kusahau Msondo ambayo hutumbuiza hapo kila Alhamisi.

Kwa upande wa Kisuma Bar iliyopo Mbagala Sabasaba, Talent Band hupatikana kila Jumamosi huku pia ikipatikana Kisuma ya Mbagala Rangi tatu kila Alhamsi. Msondo wao hupatikana Kisuma ya Sabasaba kila Ijumaa.

No comments