MOURINHO ASEMA LUKAKU ANGEGHARIMU PAUNI MIL 150 KAMA MAN UNITED WANGEZEMBEA KUMSAJILI MAPEMA


Jose Mourinho anaamini kuwa Romelu Lukaku angeigharimu Manchester United pauni milioni 150 kama wangechelewa kumsajili hadi Neymar alipoijunga na PSG.

Wakati United ililipa pauni milioni 75 kumsajili Lukaku kutoka Everton, PSG ilivunja rekodi ya dunia kwa kulipa pauni milioni 198 ili kumnasa Neymar.

Mourinho anasema kama wangechelewa kumsajili Lukaku hadi siku ya kufunga dirisha la usajili, basi anaamini wangelazimika kulipa hata mara mbili ya malipo waliyofanya.No comments