Habari

MOURINHO SASA AUKUBAKI ‘MUZIKI’ WA ANTHONY MARTIAL

on

Kocha wa Manchester United Jose Mourinho amesema winga wake Anthony Martial ameimarika na ameanza kuonyesha vitu adimu uwanjani. 
Martial aling’ara sana Old Trafford katika msimu wake wa kwanza chini ya Luis van Gaal, lakini akawa na wakati mgumu msimu uliofuata wakati Mourinho aliposhika usukani wa klabu hiyo.
Mara kadhaa Mourinho alimkosoa  nyota huyo wa Kifaransa, hali iliyoonekana kumchanganya na kumpotezea uwezo wa kujiamini.
Hata hivyo msimu huu ameibuka upya na licha ya kuwa anatokea benchi katika mechi nyingi, lakini tayari ameshapachika magoli maane huku akiwa tishio kwa mabeki wa timu pinzani kila anapoingia uwanjani.
Mourinho amesema: “Naona maendeleo makubwa kwake, kimwili, kiakili na kisoka. Ni mwenye furaha ana anafanya vizuri sana.
“Anatokea benchi na  kama ni kwa dakika 10 zilizobakia, bado ataufurahia mchezo na kujituma kuhakikisha anachangia ushindi.”

Comments

comments

About Saluti 5

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *