MPINZANI WA GENEVIEVE NNAJ ASEMA UKUBWA WA JINA LAKE HAUMUELEMEI HATA KIDUCHU

STAA mwenye mvuto nchini Nigeria ambaye anatajwa kuwa na upinzani na Omotola Jalade, Genevieve Nnaj, amesema kuwa hajawahi kusumbuliwa na ukubwa wa jina lake.

Staa huyo amesema, kwanza haoni kama kuna mabadiliko yoyote kabla ya kuanza sanaa na hivyi sasa alipoanza kujihusisha na masuala ya uigizaji.

“Naweza nisieleweke sana lakini binafsi sioni kama kuna tofauti kubwa kwenye jamii kabla sijaanza kuigiza na haya maisha yangu ya sasa,” alisema.


“Ni suala la kujipanga tu. Kama utakuwa shabiki wa mitandao ya kijamii ni dhahiri hili suala lazima likukumbe,” aliongeza.

No comments