MSAFIRI DIOUF ATUA BONGO KWA MAPUMZIKO …kuachia tatu mpya


Rapa na mwimbaji wa zamani wa Twanga Pepeta Msafiri Diouf ambaye kwasasa anafanya muziki London, Uingereza, amerejea Bongo kwa mapumziko mafupi.

Diouf ameiambia Saluti5 kuwa aliingia Dar es Salaam juzi usiku na anatarajiwa kuwa hapa nchini kwa muda usiopungua mwezi mmoja.

“Mwaka jana nilikuja na kukaa kwa wiki tatu, safari hii natarajia kukaa angalau kwa mwezi mmoja na wiki moja au mbili,” alisema Diouf.

Mwanamuziki huyo anasema hajaja mikono mitupu bali atakuwa na zawadi ya nyimbo tatu mpya atakazozirekodi hapa Dar es Salaam ndani ya siku chache zijazo.

Wiki ijayo Diouf ataingia studio za C9 Records kufyatua wimbo wa kwanza uliopewa jina la “The Bridge”.

Saluti5 ilikuwepo C9 Records wakati Diouf akifanya ‘booking’ ya kurekodi ngoma hiyo ya “The Bridge” ambayo amesema itakuwa na vionjo vya reggae.
Msafiri Diouf (kulia) akiwa na producer C9 ndani ya C9 Records  
 Msafiri Diouf 
Msafiri Diouf  akiwa mwenye furaha nyingi

No comments