MSUVA ASEMA TSHISHIMBI NDIYE ATAKAYEIPA YANGA UBINGWA MSIMU HUU

WINGA wa wa zamani wa Yanga, Simon Msuva amehamishia mabao yake akiifungia Taifa Stars juzi mabao mawili lakini akasema amehangalia mikanda ya mechi mbili za Yanga kisha akasema huyu Papy Tshishimbi ni mtu atakayeipa ubingwa timu yake hiyo ya msimu huu.

Akiongea mapema jana, Msuva amesema ameangalia mechi ya Yanga dhidi ya Simba kisha akafanya hivyo tena katika mchezo wa kwanza wa Ligi dhidi ya Lipuli na kugundua kwamba usajili wa Tshishimbi ni moja ya alama tosha zitakazoipa mafanikio makubwa timu yake hiyo.

Msuva alisema ujio wa Tshishimbi umeongeza nguvu kubwa katika safu ya kiungo ya Yanga na kwamba safu ya ushambuliaji itakuwa na nafasi kubwa na kufunga mabao mengi.

Alisema kiungo huyo ameonyesha uwezo mkubwa na kwamba endapo angekuwa bado katika kikosi hicho, angeongeza nguvu zaidi na kwamba Wanayanga watulie watapata ubingwa.

“Naifuatilia sana Yanga katika kila mchezo, hii ni timu yangu na nataka nikwambie katika kitu ambacho viongozi wamenifurahisha ni usajili wa Tshishimbi, huyu jamaa anajua,” alisema Tishishimbi.

“Nimemwangalia katika mechi kama mbili nikagundua kwamba huyu jamaa anajua kupiga pasi kali, hasa juhudi zake huwezi kusema ni mgeni kama hujaambiwa, nafikiri washambuliaji watafaidi sana hizi pasi zake.”

No comments