MWIGIZAJI OMOTOLA JALADE ASEMA ANAVUTIWA PIA NA FANI YA MUZIKI

STAA wa filamu nchini Nigeria, Omotola Jalade amesema kuwa pamoja na fani ya uigizaji pia amekuwa akivutiwa na kazi za muziki ambazo zinafanywa na watoto wake ambao ni Captain E na Kiss Daniel.

Omotola amesema kuwa amekuwa akifuatilia kila hatua inayoendelea kwa watoto hao ili kuwasaidia kufikia ndoto yao ya kuwa mastaa wakubwa kimuziki.

Watoto hao wa kiume wote wamevutiwa na kazi za muziki huku Captain E akionekana kuwa mbali zaidi baada ya kuanza kujifunza namna ya kutengeneza kazi zake mwenyewe studio.


“Nafanya uigizaji lakini hata muziki pia navutiwa nao na hasa kazi zinazofanywa na vijana wangu,” alisema staa huyo wakati alipokuwa akijibu maswali ya mashabiki wake kupitia mitandao ya kijamii.

No comments