NE-MO AJA KIVINGINE KUISHIKA RnB YA BONGO KWA WIMBO MKALI “KIPOTABO”


MSANII wa  muziki wa kizazi kipya Shaban Mpute 'Ne-Mo' (pichani) amesema amedhamiria kurudi katika familia ya muziki kivingine, huku akitarajia kuachia wimbo wake mpya unaitwa 'Kipotabo' Septemba 19 mwaka huu.

Akizungumzia ujio wake huo mpya  Ne-Mo chini ya lebo ya 'Digital City Drimz'  alisema kuwa  amedhamiria kuirejesha RnB ya Bongo katika viwango na pia kuipeleka nje ya mipaka ya Tanzania, kwa sababu anahifahamu vizuri.

Alisema kwa sasa kuna wasanii kama Diamond Platnumz, Ali Kiba, Vanessa Mdee, Navy Kenzo na wengineo wameubeba muziki wa Bongofleva na kusaidia kuupenyeza kimataifa, naye ana matumaini makubwa ya kufika walipo wasanii hao.

Alisema nyimbo yake hii mpya inayokwenda kwa jina la 'Kipotabo' ambayo imetengenezwa katika studio za  Combination Sound  chini ya mtayarishaji Man Water na video inakuja kipitia Kwetu Studio.

Ne-Mo amesema ukimya wake umetokana na masomo ambapo aliamua kutulia amalizie masomo ya 'Mass Communication' kabla ya kuendelea harakati za muziki. 

Meneja wa Ne-Mo,  Habibu Anga 'Guru Picasso' ameiambia Saluti5 kuwa Jumatatu ijayo wataachia rasmi wimbo  wa “Kipotabo”.

Alisema Ne-mo alikuja kuitikisa zaidi Tanzania na Afrika Mashariki mwaka 2013 alipoanchia wimbo uliokwenda kwa jina la "Number One" ambao alimshirikisha mkali mwenzake Ommy Dimpoz.

Baada ya mafanikio makubwa ya wimbo huu wa 'Number One' Ne-Mo hakuwahi kutoa kazi yake nyingine yoyote ile, zaidi ya nyimbo za kushikishwa ambazo ni  'Mrs Superstar' ya Young Killer, 'Tulikuwepo' ya Niki Mbishi na 'Sijutii' ya Msamiati.No comments