Nemanja Matic anaamini Manchester United inahitaji kushinda mechi kama za  Stoke City iwapo inahitaji kutwaa taji la Premier League.

Kikosi cha Jose Mourinho kilianza msimu kwa kishindo na kushinda mechi zote tatu za mwanzo lakini ikawa na wakati mgumu pale iliposafiri kwenda bet365 Stadium, Jumamosi na kuambulia sare ya 2-2 dhidi ya Stoke City.

"Ulikuwa mchezo mgumu,"  kiungo huyo mkabaji aliiambia MUTV. "Siku Stoke City imekuwa ngumu kwenye uwanja wake wa nyumbani. Ni timu ngumu ili tulazimu kuambulia pointi moja.

"Iwapo tunataka kutwaa ubingwa ni lazima kushinda mechi kama hizi."USISAHAU KUBONYEZA SUBSCRIBE HAPO
LIKE PAGE YETU YA FACEBOOK Saluti5

Post a Comment

 
Top
Nicolaus Trac