NEW AUDIO: “YANANITESA” NYIMBO MPYA YA MAPACHA WATATU ORIGINAL
Hii ni ndiyo kazi ya kwanza ya bendi ya bendi ‘mpya’ ya Mapacha Watatu Original chini yake Khalid Chokoraa.

Wimbo unakwenda kwa jina la “Yananitesa”, kazi nzuri yenye urefu wa dakika 4.30 iliyorekodiwa katika studio za On Time Production, mkono wake producer Amoroso Soundo.

Safari ya wimbo huu inaanzia Twanga Pepeta ambapo Chokoraa aliutunga na kuurekodi na kuupa jina la “Prison Love” na baadae kubadilishwa kuwa “Yananitesa” lakini hadi anahama bendi, bado kigongo hicho kilikuwa hakijaachiwa hewani.

Baada ya Chokoraa kuanzisha Mapacha Watatu, akaufanyia marekebisho madogo sana na ndiyo huu sasa unawajia huku kukiwa bado na gitaa la God Kanuti, sauti za Mirinda Nyeusi, Ally Chocky na Star Boy wote kutoka Twanga Pepeta.

Sauti pekee iliyoondolewa ni ya Haji Ramadhan Makuke na badala yake ikaingizwa ya Frank Kabatano lakini katika melody ile ile aliyoitengeneza Haji.

Isikilize hapo juu nyimbo hiyo tamu kutoka kwa Mapacha Watatu Original.

No comments