NEYMAR AFICHUA SABABU ZA KUITEMA BARCELONA NA KUJIUNGA NA PSG


NEYMAR amedai kuwa ameitema Barcelona na kujiunga na Paris Saint-Germain kwaajili ya kushinda taji la Champions League.
Mshambuliaji huyo wa Brazil amesema PSG ina nafasi kubwa ya kutwaa Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu huu.
Neymar mwenye umri wa miaka 25 amesema: "Moja ya sababu zangu kubwa za kujiunga na PSG ni kuisaidia kuandika historia. Champions League sio taji pekee tunalotaka kushinda - lakini ni taji muhimu sana.
"Lengo kuu msimu huu ni kujaribu kunyakua taji - hiyo ndiyo hadhi ya klabu hii kwa sasa. Nina amini tuna kikosi bora cha kufanya hivyo".

No comments