Habari

NEYMAR AOMBA RADHI PSG, CAVANI ASEMA HANA TATIZO …KOCHA ASHINDWA KUTOA MAAMUZI MAGUMU

on

Mwanasoka ghali duniani Neymar ameomba radhi wachezaji wenzake Paris Saint-Germain kufuatia mvutano wake na Edinson Cavani wiki iliyopita katika mchezo dhidi ya Lyon.
Neymar na Cavani walizinguana juu ya nani apige mipira ya adhabu kwenye uwanja wa Parc des Princes ambapo PSG ilishinda 2-0.
Kufuatia mzozo huo, gazeti moja la Hispania likaibuka na habari kuwa Neymar ametoa shinikizo kwa wamiliki wa PSG kwamba anataka Cavani auzwe.
Kocha wa PSG Unai Emery amesema wote Neymar na Cavani wataendelea kubeba jukumu la kupigia penalti, lakini Mhispania huyo akakataa kuweka wazi ni nani ndiye chaguo namba moja.
Kwa upande wake, Cavani amesema hana tatizo na Neymar aliyewasili kutoka Barcelona kwa pauni milioni 198.
Cavani amekiambia kituo cha radio cha Uruguay Gol de Medianoche de Radio Universal: “Nimesikia watu wakisema kuwa sitakubali mtu mwingine apige penalti na kwamba nina matatizo na Neymar, huo ni uzushi.
“Ukweli ni kwamba hakuna tatizo, Neymar ndiyo kwanza amewasili na kama nilivyosema hapo awali, tutajitahidi kumfanya azoee mazingira mapya kwa haraka”.
Jana wachezaji hao walishiriki mazoezi ya PSG na hali ilionekana kuwa shwari.

Comments

comments

About Saluti 5

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *