Habari

NEYMAR NA CAVANI BIFU LAO HALIKUISHIA UWANJANI, UGOMVI ULIKWEND HADI VYUMBANI

on

Neymar na Edinson Cavani walilazimika kutengenishwa na wachezaji wenzao wa Paris Saint-Germain kufuatia mgogoro wao wa kugombea kupiga mipira ya adhabu.
Washambuliaji hao wawili wa bei mbaya walionekana kuwa pacha hatari kwenye safu ya ushambuliaji ya PSG, lakini sasa hali inaanza kutishia amani baada ya kila mmoja kutaka ‘ufalme’.
Katika ushindi wa 2-0 dhidi ya Lyon, Jumapili, nyota hao walibishana mara mbili juu ya nani apige mipira ya adhabu. 

Cavani alitaka kupiga mpira wa adhabu, lakini beki Dani Alves akampora mpira na kumpa Neymar ambaye alipiga free-kick hiyo ambayo haikuzaa matunda.

Baadaye PSG wakapata penalti, Neymar akataka kupiga, lakini Cavani akagoma na kupiga yeye na kwa bahati mbaya penalti hiyo nayo haikuzaa matunda.

Gazeti la kila siku la Ufaransa L’Equipe linadai Neymar na Cavani walikwaruzana baada ya mchezo.
Kwenye ukurasa wake wa mbele, gazeti hilo limedai kuwa bifu la Neymar na Cavani lililoanzia uwanjani, liliendelea hadi katika vyumba vya kubadilishia nguo na ilibidi waamuliwe na wachezaji wenzao.

Comments

comments

About Saluti 5

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *