NGAO YA HISANI YA SIMBA YAREJESHWA TFF KWA MAREKEBISHO

HATIMAYE  Shirikisho la soka Tanzania (TFF), limefanya marekebisho katika Ngao ya Jamii waliyoshinda Simba.

Simba walikabidhiwa Ngao ya Jamii baada ya kuifunga Yanga kwa mikwaju ya 5-4 ya penati, lakini ikawa na makosa katika maandishi.

Ngao hiyo ilikuwa imeandikwa “Community Sheild” badala ya “Community Shield”.

Baada ya malalamiko kuwa makubwa, TFF iliiomba Simba kuirudisha Ngao hiyo kwa ajili ya marekebisho.

No comments