NICHOLAS GYAN AREJEA NCHINI AKIWA FITI KUITUMIKIA SIMBA SC

MSHAMBULIAJI wa Simba raia wa Ghana, Nicholas Gyan amerejea nchini mapema leo akiwa tayari kwa ajili ya kazi ya kuitumikia Simba.

Afisa Habari wa Simba, Haji amesema kupitia ukurasa wake wa Instagram kuwa Gyan aliyekuwa mfungaji bora katika klabu yake ya Ebusua ya Ghana na katika Ligi Kuu, amerejea wikiendi hii.


Amesema kuwa mshambuliaji huyo amerejea rasmi kuanza kuitumikia Simba na kama benchi la ufundi la timu hiyo chini ya kocha Joseph Omog litaona kama anaweza kucheza mechi dhidi ya Azam mwanasoka huyo anaweza kucheza.

No comments