"NIKIMUONA" YA PEACE MAPEPE KUANIKWA RASMI IJUMAA HII

MKALI wa Bongofleva, ‘Peace Mapepe’ amesema kuwa mkakati wake mkubwa katika muziki ni kuhakikisha anafika mbali zaidi na kutambulika hadi nje ya mipaka ya nchi na kujijengea jina zaidi.

Kesho Ijumaa Peace Mapepe anatarajiwa kuachia ngoma yake mpya inayokwenda kwa jina la ‘Nikimuona’ ambayo imebeba ujumbe mnono wa kimapenzi, ambayo mwenyewe anadai itakuwa funika bovu.

“Nawaomba mashabiki wa muziki wa bongofleva kukaa mkao wa kusubiri ujio wangu mpya katika kibao ‘Nikimuona’ ambacho naamini kitakuwa gumzo kubwa nitakapokiachia rasmi,” amesema Peace.


Kabla ya kuibuka na wimbo huo, Peace ambaye pia ni mtaalam wa kutengeneza vipodozi na dawa za ngozi kwa kutumia matunda na vitu vingine vya asili, alifanya vyema na ngoma kadhaa zikiwemo zile mbili za ‘Macho Kodo’ na ‘Mdundiko’.

No comments