NYOSHI ASEMA UMBEYA MWISHO MIAKA 40, UKIZIDI HAPO UTAZIKWA NAO


Mwimbaji wa zamani wa FM Academia, Nyoshi el Saadat “Rais wa Vijana” amesema hakuna kitu kibaya umbeya na unafiki kuweka kambi kwenye akili ya mtu mzima.

Nyoshi anasema kwa bahati mbaya sana, hali hiyo imekithiri kwa wanamuziki ambao wengi wao wanakuwa wanafiki hadi uzeeni, jambo ambalo linadumaza maendeleo.

Katika maongezi yake na Saluti5, Nyoshi akasema umbeya mwisho miaka 40, ukiendelea kuwa mbeya hadi umevuka umri huo basi ujue utaendelea kuwa mbeya hadi siku ya kufa.

“Ukifika miaka 35 jitathimini sana tabia yako na hata maendeleo yako, ukifika miaka umri wa miaka 40 basi ujue uwezekano wa kubadilika ni mdogo sana, hiyo ndiyo fainali yako,” alisema Nyoshi.

Msanii huyo akasema miongoni mwa vitu vinavyorudisha nyuma soko la muziki hapa nchini, unafiki miongoni mwa wanamuziki na kwa bahati mbaya sana, wengi wanazeeka na umbeya wao.

No comments