OBREY CHIRWA: YANGA HAIWEZI KUPOTEZA POINTI KWA SABABU YANGU

MSHAMBULIAJI wa Kimataifa Obrey Chirwa  raia wa Zambia amesema kuwa klabu ya Yanga ina kikosi kipana hivyo kukosekana kwake uwanjani haiwezi kuwa sababu ya kupoteza pointi muhimu.

Chirwa amesema kuwa mashabiki wanasahau kwamba msimu uliopita wapo nyota muhimu ambao walikosekana uwanjani kwa sababu ya majeruhi lakini bado Yanga iliweza kubeba ubingwa wa Ligi Kuu bara kwa mara ya tatu.

"Naomba ijulikane kuwa mimi ni sehemu ya Yanga lakini sio mkubwa kuliko Yanga yenyewe, hivyo kukosekana kwangu uwanjani hakuwezi kuzuia mipango ya timu kusonga mbele,’’ alisema nyota huyo.

"Ni suala la kimichezo kukosekana uwanjani kwa sababu ya adhabu au hali ya majeruhi, lakini hilo haliwezi kurudisha nyuma jitihada za timu kupata matokeo mazuri uwanjani,’’ aliongeza Chirwa.

"Tuna kikosi kipana ambacho kinaweza kupambana na timu yoyote kwenye Ligi, naamini katika mechi zijazo kila kitu kitakuwa sawa na mashabiki watapata kile wanachotarajia toka kwetu."

"Nashukuru matatizo yangu yamemalizika na hata hali yangu kiafya imeanza kuimalika nitajitaidi kupambana kwaajili ya klabu yangu katika mechi zijazo," alimaliza.

No comments