OJM FILM WAANZA KUUZA UPYA MUVI ZAO ZA NYUMA

KAMPUNI ya OJM Film Company imeamua kuanza kuuza upya kazi zao za zamani ili kukidhi matakwa ya mashabiki wao waliowaomba kufanya hivyo.

Akiongea na Salutimwandishi wetu jijini Dar es Salaam jana, bosi wa OJM Film, Omary Mmaka amesema kuwa wapenzi na mashabiki wao wengi wamewaomba kurudia kuuza kazi zao hizo ambazo wamezimiss kwa muda mrefu.

“Tayari tumeanza kudurufu nakala za baadhi ya muvi zetu ambazo zilionekana kufanya vyema zaidi na tunashukuru mashabiki wanazipokea kwa mikono miwili kwa kujitokeza kuzinunua kwa wingi,” amesema Mmaka ambaye pia ni kati ya matabibu bingwa wa kijadi.


Mbali ya kuanza kurudia kudurufu kazi zao za nyuma, kampuni ya OJM Film pia iko katika harakati za kuachia Tamthilia yao ya kwanza, ambayo hata hivyo bado haijapewa jina, ambayo itashirikisha nyota wengi wa muvi za Kibongo.

No comments