OKWI SASA YUKO GADO KUWAGONGA MWADUI FC

MSHAMBULIAJI wa Simba, Emmanuel Okwi yuko fiti kupambana katika mechi ya Jumapili hii dhidi ya wachimba almasi wa Mwadui FC kwenye uwanja wa Uhuru, jijini Dar es Salaam.

Habari kutoka katika kambi ya Simba zinasema kuwa Okwi anaendelea vizuri baada ya kupata ajali kwa kugongana na kocha wake, Joseph Omog wakati wa mazoezi.

Wawili hao waligongana katika mazoezi ya vitendo wakati Simba wakiwa wanaendelea na mazoezi yao kwenye uwanja wa Uhuru kujiandaa na mechi yao dhidi ya Mwadui.

Baada ya tukio hilo lisilo la kawaida, kocha msaidizi wa wekundu hao, Jackson Mayanja na baadhi ya wachezaji wa Simba walimtoa Okwi ambaye hata hivyo baadae imeelezwa kuwa hakupata maumivu makali.


Mmoja wa maofisa wa Simba ameeleza kuwa Omog alikuwa akisikia maumivu ya kichwa hata baada ya mazoezi na alikuwa amefungwa plasta kichwani.

No comments