PELE ASEMA NEYMAR ALIKUWA SAHIHI KUONDOKA KWENYE KIVULI CHA MESSI BARCELONA


Mchawi wa soka duniani, Pele amepongeza uamuzi wa Neymar kutimka Barcelona na kuhamia Paris Saint-Germain.

Pele, 76, amesema nyota huyo mwenye umri wa miaka 25 alistahili kuondoka Barcelona ili kujitoa kwenye kivuli cha Lionel Messi.

"Kwa sasa Neymar ndiye mchezaji bora zaidi Brazil na nadhani kuondoka kwake Barcelona ni sahihi kwa vile pale alikuwa na ushindani mkubwa na Lionel Messi," anaeleza Pele.

"Ilikuwa ni jambo jema kwake kuondoka kwenda sehemu atakayokuwa huru kuonyesha uwezo wake alionao," aliongeza Pele katika mazungumzo yake na gazeti la Marca la Brazil.

No comments