Habari

PEP GUARDIOLA AMUUNGA MKONO JOSE MOURINHO

on

PEP GUARDIOLA amemuunga mkono mpinzani wake wa siku nyingi Jose Mourinho juu ya michuano ya Carabao Cup (EFL).
Mourinho kocha wa Manchester United alisema wiki hii kuwa anadhani Carabao Cup inadhohofisha nguvu za vilabu vya England katika michuano ya Ulaya.
Guardiola – ambaye timu yake ya Manchester City nayo imetinga mzunguko wa nne wa michuano hiyo – anaona kuna jambo la msingi juu ya maoni hayo.
Alipoulizwa kama anakubaliana na mtazamo wa Mourinho, Pep alisema: “Maoni yangu ni sawa na yake. Hivyo biashara ni biashara. Tuna mechi nyingi sana.
“Kama unalazimika kushiriki michuano, ni lazima ucheze. Ni nzuri kwa wachezaji ambao huwatumii sana. Ni taji ambalo ukishinda ni jambo jema lakini baada ya hapo watu hawalipi heshima kubwa.
“Nadhani ni taji zuri kushinda pale unaposhinda sambamba na mataji mengine, lakini unatumia nguvu ngingi sana”.
Kikosi cha Guardiola kilichuana na West Brom katikati ya wiki na kocha huyo analalamikia ratiba ilivyo – kwamba unacheza dakika 90 kisha timu inasafiri kwa bus kwa saa tatu hadi nne halafu siku tatu baadae ichuane na Crystal Palace, siku tatu tena Shakhtar Donetsk, siku tatu au nne safari ya Stamford Bridge kuikabili Chelsea.
“Kwa makocha tunapoteza nguvu ngingi,” alisema Guardiola.

Comments

comments

About Saluti 5

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *